[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Eli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Jan Victors (1645) ukimuonesha Anna alipomtolea Samueli kwa Eli, aliyeketi kulia.
Eli na Samueli walivyochorwa na John Singleton Copley, (1780).

Eli (kwa Kiebrania עלי ʻEli, ʻĒlî) alikuwa kuhani wa Israeli kwenye hekalu la Shilo kadiri ya Kitabu cha Kwanza cha Samueli.

Ndiye aliyemlea Samueli mwenyewe baada ya huyo kuachishwa ziwa na kutolewa na mama yake amtumikie Mungu maisha yake yote.

1Sam 3 inasimulia wito wa mtoto huyo: akiwa amelala karibu na sanduku la agano akaamshwa na Mungu mara tatu mpaka akafundishwa na Eli kumtambua na kumuitikia Mungu. Hapo akamtabiria Eli adhabu kali, na hivyo Israeli ikajua kuwa amefanywa nabii wa Bwana.

Kulingana na utabiri huo Waisraeli walishindwa na Wafilisti vitani, wana 2 wa Eli waliuawa katika mapigano na Eli alikufa kwa mshtuko na sikitiko alipopata habari.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eli kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.