[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Daa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Daa
Daa-damu kutoka Ulaya (Marphysa sanguinea)
Daa-damu kutoka Ulaya (Marphysa sanguinea)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Nusuhimaya: Eumetazoa (Wanyama wenye tishu za kweli)
Faila ya juu: Lophotrochozoa
Faila: Annelida (Wanyama kama nyungunyungu)
Ngeli: Polychaeta
Ngazi za chini

Nusungeli 4:

Daa, choo au mwata ni wanyama wa bahari (spishi kadhaa kwenye maji matamu na nchi kavu) ya ngeli Polychaeta ya faila Annelida (anelidi). Spishi nyingi sana huishi katika mashapo ya sakafu ya bahari au matope ya maziwa na mabwawa, na spishi zinazoishi karibu na pwani hutumika kama chambo cha kuvulia samaki. Spishi nyingine huogelea huru majini na kadhaa zinatokea katika maeneo manyevu ya nchi kavu. Spishi zinazotumika kama chambo huitwa daa kwa kawaida, lakini inapendekezwa kutumia jina hili kwa spishi zote za Polychaeta.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]