Goguryeo
Ufalme wa Korea Goguryeo |
---|
|
Goguryeo ni nasaba ya kwanza ya Korea ya kale ambayo ilianzishwa na Jumong (주몽朱蒙) mnamo 37 KK. Ilianzishwa karibu na eneo la mto Dongga (동가강佟佳江) ambapo ni tawi mkondo wa Abrok (압록강). Korea inajivunia sana Goguryeo kama mwanzo wa taifa la Korea.[1]
Kuundwa na Uenezi wa Goguryeo
[hariri | hariri chanzo]Hadithi ya kuzaliwa kwa taifa inaeleza kwamba Jumong alizaliwa nje ya yai na kulelewa na mfalme Kuemywa (금와왕) wa Buyeo Mashariki (동부여). Jina la Jumong, linamaana ya mtu mwenye uwezo mkubwa wa kupiga mishale. Kama jinsi jina linavyoonyesha, alikuwa mkali katika mishale na kwa sababu ya uwezo wake, mtoto wa mfalme Daeso (대소왕자) alimwonea gele sana Jumong. Kwa hiyo, Jumong akajionea tabu na kuamua kutoroka Buyeo Mashariki akiwa na marafiki zake watatu. Akaenda zake huko Jolbon Buyeo (졸본부여) na kumwoa Bi. Sosuno (소서노) ambaye alikuwa binti wa mfalme katika taifa hilo. Jumong akarithi ufalme na kubadili jina la nchi na kuliita Goguryeo baada ya jina la mzee wake.
Tangu mfalme wa kwanza, mfalme Dongmyungsung (동명성왕), Goguryeo ilivamiwa kivita mara kadhaa na nchi kama Han (한나라), kabila la Sunbi (선비족). Lakini, kwa utawala wa mfame wa 11, Gogurye ilifanikiwa kuipola mamlaka nchi kama Yodong (요동). Hadi kipindi cha mfalme wa 24, ilikuwa na waziri wake mkuu, ikapanua safu ya nchi yake na kutimua mashambulizi yote kutoka nje. Mfalme maarufu ni Guangaeto (광개토대왕).
Kuangamizwa kwa Goguryeo
[hariri | hariri chanzo]Hata hivyo, wakati ipo chini ya utawala wa mfalme wa 27, Youngryou (영류왕), Goguryeo ilionekana kama imejisalimisha kwa Dang (당나라) kwa hiyo mfalme akauawa na Yoengaesomoon (연개소문) na mfalme Bojang (보장왕) akarithi cheo. Baada ya kufa kwa Yoengaesomoon, watu wakawa hawashirikiani na taifa lao vizuri na kupelekea taifa kuwa dhaifu, lilikuja kuangamizwa na nguvu ya muungano baina ya Shinla (신라) na Dang.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Goguryeo. Proud History of Korea". www.mygoguryeo.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-26. Iliwekwa mnamo 2009-06-12.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- [1] Archived 1 Oktoba 2016 at the Wayback Machine.