[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Adidas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Xbox Games early 2019
Xbox Games late 2022

Adidas (nembo adidas ilichorwa mwaka 1949) [1] ni shirika la kimataifa la Ujerumani, lililoanzishwa na lenye makao yake makuu huko Herzogenaurach, Bavaria, ambalo husanifu na kutengeneza viatu, nguo na vifaa. Ni mtengenezaji mkubwa zaidi wa nguo za michezo huko Uropa, kampuni ya Adidas ni ya pili kwa ukubwa ulimwenguni, baada ya Nike, Inc.. [2] [3] Ni kampuni inayomilikiwa na Kundi la Adidas, ambalo lina hisa 8.33% katika klabu ya soka Bayern Munich, [4] na Runtastic ambayo ni kampuni ya teknolojia ya siha ya Austria. Mapato ya Adidas kwa mwaka 2018 yameorodheshwa kuwa ni Uro €21.915 bilioni.

Kampuni ya Adidas ilianzishwa na Adolf Dassler katika nyumba ya mama yake, alijiunga na kaka yake mkubwa Rudolf mnamo mwaka 1924 chini ya jina Gebrüder Dassler Schuhfabrik ("Dassler Brothers Shoe Factory"). Dassler alisaidia katika ukuzaji wa viatu vya kukimbia vilivyoitwa ( spikes ) kwenye hafla nyingi za riadha. Ili kuimarisha ubora wa viatu vya riadha vilivyoinuka, alihama kutoka kwa mtindo wa awali wa spikes nzito hadi kutumia turubai na raba. Dassler alimshawishi mwanariadha wa Marekani Jesse Owens kutumia kiatu cha (spikes) aliyoitengeneza kwa mikono yake kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya 1936 . Mnamo 1949, kufuatia kuvunjika kwa uhusiano kati ya ndugu, Adolf aliunda Adidas na Rudolf alianzisha Puma, ambayo ikawa mpinzani wa biashara wa Adidas.

Mistari hiyo mitatu ni alama ya utambulisho wa Adidas, ambayo imetumika kwenye miundo ya nguo na viatu vya kampuni kama msaada wa masoko. Chapa, ambayo Adidas ilinunua mwaka wa 1952 kutoka kwa kampuni ya michezo ya Karhu Sports kwa gharama ya €1,600 na chupa mbili za whisky, [5] [6] ilifanikiwa sana hivi kwamba Dassler aliielezea Adidas kama "Kampuni ya mistari mitatu". [5] [6]

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adidas kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "The History of Adidas". On This Day In Fashion. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Machi 2013. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Adidas, Deutsche Telekom, Infineon: German Equity Preview". Bloomberg L.P. 16 Januari 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Novemba 2012. Iliwekwa mnamo 31 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Ranking of the largest sporting goods manufacturers worldwide in 2009, based on revenue". Statista.com.
  4. "Allianz steigt nach Adidas und Audi beim FC Bayern München ein". Autohaus.de (kwa Kijerumani). 2014-02-13. Iliwekwa mnamo 2021-12-28.
  5. 5.0 5.1 Smit, Barbara (2007). Pitch Invasion, Adidas, Puma and the making of modern sport. Penguin. uk. 44. ISBN 978-0-14-102368-7.
  6. 6.0 6.1 Chadwick, Simon; Arthur, Dave (2007). International Cases in the Business of Sport. Butterworth-Heinemann. uk. 438. ISBN 978-0-7506-8543-6.