[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Ando Masahashi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ando Masahashi
muhusika wa Heroes
Mwonekano wa kwanza "Genesis"
Mwonekano wa mwisho "Brave New World"
Imechezwa na James Kyson Lee
Maelezo
Majina mengine Crimson Arc
Kazi yake Shujaa wa kukodiwa
Ndoa Kimiko Nakamura (mchumba)
UwezoKukuza nguvu
Mvurumisho wa nishati

Ando Masahashi (安藤 マサハシ) ni jina la kutaja uhusika wa kipindi cha mfululizo wa televisheni unaorushwa hewani na kituo cha NBC, Heroes. Uhusika umechezwa na James Kyson Lee.[1] Uhusika uliwekwa kama uhusika wa chini wa msimu wa kwanza, na ukaja kupandishwa hadi kuwa uhusika wa kawaida kwenye msimu wa pili wa mfululizo.[2] Ametambulishwa kwa watazamaji wa televisheni katika sehemu ya kwanza ya mfululizo “Genesis[3] akiwa kama mwajiriwa katika kampuni ya Yamagato Industries, Ando ni rafiki wa karibu na mfanyakazi mwenzake Hiro Nakamura katika safari kadhaa za kukoa dunia.

Mara kwa mara huishinda hali ya kutokuwa na usalama kwa kuthaminiwa kiasi hasa kwa kufuatia hali yake ya kutokuwa na nguvu za kipekee kama wahusika wengine na kumwangazia Hiro kuwa kama mkombozi wake. Mwishoni mwa msimu wa tatu, "Villains", anapata uwezo wa kuongeza nguvu za ziada kwa kitu chochote anachokigusa hasa vile vilivyokosa nguvu.

  1. "Heroes Official Website". NBC. Iliwekwa mnamo 2008-11-17.
  2. "Exclusive Interview: James Kyson Lee of Heroes". heroesrevealed. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-13. Iliwekwa mnamo 2008-11-17.
  3. ""Heroes" Chapter One 'Genesis' (2006)". IMDB. Iliwekwa mnamo 2008-11-17.