Şalom
Mandhari
Şalom (Kiebrania: "שָׁלוֹם" - "Amani") ni gazeti la Kiyahudi ambalo huchapishwa kila wiki huko nchini Uturuki. Tahajia ya neno ni ya Kituruki lakini jina lenyewe ni la Kiebrania Shalom.
Lilianzishwa tarehe 29 Oktoba, 1947 na mwandishi wa habari wa Kituruki-Kiyahudi Avram Leyon. Linachapishwa mjini Istanbul. Lugha yake ni Kituruki lakini huwa pia na ukurasa moja kwa Ladino. Yakup Barokas ni mhariri wake. Mzunguko wake ni karibu 5,000.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Şalom (Kituruki)
- Şalom (Ladino) Archived 11 Desemba 2008 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Şalom kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |