Google Authenticator huimarisha usalama wa akaunti zako mtandaoni kwa kuongeza hatua ya pili ya kuthibitisha unapoingia katika akaunti.
Hii ina maana kuwa, kando na nenosiri lako, utahitaji pia kuweka msimbo uliozalishwa na programu ya Google Authenticator kwenye simu yako.
Msimbo wa kuthibitisha unaweza kuzalishwa na programu ya Google Authenticator kwenye simu yako, hata bila mtandao au muunganisho wa mtandao wa simu.
* Kusawazisha misimbo yako ya Authenticator kwenye Akaunti yako ya Google na katika vifaa vyako vyote. Hii inakuwezesha kuifikia wakati wowote hata ukipoteza simu yako.
* Kuweka mipangilio ya akaunti zako kiotomatiki kwenye Authenticator kwa kutumia msimbo wa QR. Hii ni haraka na rahisi, na husaidia kuhakikisha kuwa misimbo yako ya kuthibitisha imewekwa ipasavyo.
* Kudhibiti akaunti nyingi. Unaweza kutumia programu ya Authenticator kudhibiti akaunti nyingi, kwa hivyo huhitaji kubadilisha programu kila wakati unapohitaji kuingia katika akaunti.
* Kuzalisha misimbo ya kuthibitisha inayotumika ndani ya muda mahususi na kulingana na utaratibu unaoweza kuhesabiwa. Unaweza kuteua aina ya misimbo ya kuthibitisha inayokufaa zaidi.
* Kuhamisha akaunti kati ya vifaa kupitia msimbo wa QR. Hii ni njia rahisi ya kuhamishia akaunti zako kwenye kifaa kipya.
* Ili utumie Google Authenticator kwenye Google, unahitaji kuwasha kipengele cha Uthibitishaji wa Hatua Mbili katika Akaunti yako ya Google. Ili uanze kutumia, tembelea http://www.google.com/2step
Ilani ya ruhusa:
Kamera: Unahitaji kuruhusu ufikiaji wa kamera ili uweze kuongeza akaunti ukitumia misimbo ya QR
Ilisasishwa tarehe
6 Nov 2024