[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Pambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Surahi, Dola la Mughal, karne ya 17, Makumbusho ya Taifa, New Delhi, India.

Pambo (wingi: Mapambo kutoka kitenzi: kupamba) ni kitu au kifaa kinachotumika kuongezea urembo au uzuri wa mtu, nyumba, au kitu kingine chochote.

Tangu zamani za kale binadamu ameonyesha kipaji chake cha usanii kwa kupamba vitu mbalimbali, hasa vile vinavyomhusu zaidi, kama vile mavazi yake na mwili wake mwenyewe.

Mapambo katika ujenzi

[hariri | hariri chanzo]

Katika ujenzi na sanaa ya mapambo ni zana zinazotumika kutia nakshi eneo au kitu fulani. Mapambo kwa ajili ya majengo huchongwa kutoka kwenye mawe, mbao au vito vya thamani, udongo, au pia mengine huchorwa juu yake, k.mf. juu ya kitambaa.

Mitindo mbalimbali ya mapambo imegunduliwa kupitia sanaa na ujenzi, ikiwemo ya ufinyanzi, samani na kazi za uhunzi pia. Kwenye nguo, kuta na vitu vingine ambapo mapambo yaweza kuwa kitu pekee kinachosaidia kuwepo kwake, michoro na miundo pia hutumika zaidi.

Miundo mbalimbali inayotumika katika michoro ya mapambo hutolewa katika maumbo ya kijiometri, na maumbo ya maua, picha, michoro mbalimbali kama ya mimea na wanyama pia.

Aina za mapambo anayovalia binadamu

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu: Mapambo ya vito

Mara nyingi katika jamii, binadamu, haswa mwanamke, anapenda sana kujitia nakshi kwa mapambo yaliyotengenezwa kwa vito au hata plastiki za rangi. Hii imekuwa jambo la kawaida katika jamii. Mapambo hayo kwa wanawake wa Kiafrika ni kama vile:

  1. Herini/kipuli ni pambo linalotengenezwa kwa madini ya dhahabu, shaba au fedha linalovaliwa sikioni.
  2. Mkufu ni pambo lenye umbo la mnyororo mwembamba lililotengenezwa kwa aina fulani ya madini linalovaliwa shingoni.
  3. Kikuba kinachovaliwa nyweleni.
  4. Kipini ni kichuma chenye rangi ya dhahabu, shaba au fedha kinachovaliwa puani.
  5. Bangili ni pambo la mviringo linalovaliwa mkononi.
  6. Utaji ni ushungi unaotiwa maua ya kung'ara unaovaliwa kichwani.
  7. Kidani ni pambo linalovaliwa shingoni.
  8. Koja ni shada la mtungo mrefu wa maua au shanga linalovaliwa shingoni.
  9. Udodi ni uzi mwembamba unaotengenezwa kutokana na ngozi au chuma unaovaliwa mkononi.
  10. Kikukuni pambo linalotengezwa kwa madini ya dhabu, shaba au fedha linalovaliwa mguuni.
  11. Chupio ni kifaa cha chuma au plastiki kinachofanana na pini kinachotumiwa kubania nywele.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pambo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.