Roma
Roma (pia: Rumi) ndio mji mkuu wa Jamhuri ya Italia. Uko katika makutano ya mito ya Tiber na Aniene karibu na Bahari ya Mediteranea. Roma una wakazi milioni 2.7 katika eneo la 1285 km².
Mji wa Roma | |||
| |||
Mahali pa mji wa Roma katika Italia |
|||
Majiranukta: 41°54′N 12°30′E / 41.900°N 12.500°E | |||
Nchi | Italia | ||
---|---|---|---|
Mkoa | Lazio | ||
Idadi ya wakazi (2007) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 2.718.768 | ||
Tovuti: www.comune.roma.it |
Ndani ya mji wa Roma lipo eneo la mji wa Vatikano ambao ni nchi ya kujitawala chini ya Papa wa Kanisa Katoliki.
Historia ya mji inasemekana imeanza rasmi tarehe 21 Aprili 753 KK, lakini majengo ya kwanza ni ya karne ya 10 K.K. Katika karne za KK ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Roma, halafu wa Jamhuri ya Roma, hatimaye wa Dola la Roma. Kuanzia karne ya 7 B.K. ukawa mji mkuu wa Dola la Papa, halafu wa Ufalme wa Italia na sasa wa Jamhuri ya Italia. Huitwa mara nyingi "Mji wa Milele".
Eneo la Roma
Roma uko katikati ya Italia ikiwa mita 20 juu ya UB ndani ya tambarare ya bonde la mto Tiber linalopakana na milima ya Abruzzi, milima ya Sabino na milima ya Albani. Wilaya za jirani ni Viterbo, Rieti, L'Aquila, Frosinone na Latina. Mwanzo wa Roma ulikuwa kwenye vilima saba vilivyo katikati ya mji wa leo vinavyoitwa: Palatino, Aventino, Kapitolo, Quirinale, Viminale, Esquilini na Caeliano.
Hali ya hewa
Hali ya hewa hutawaliwa na bahari iliyo karibu. Wastani ya halijoto kwa mwaka ni sentigredi 15,4. Mvua hunyesha wastani ya mm 758 kila mwaka.
Miezi yenye joto ni Juni hadi Agosti ikiwa na wastani ya sentigredi 21 hadi 23,8 ni miezi ya mvua kidogo.
Mwezi baridi ni Januari ikiwa na wastani wa sentigredi 7,9.
Uchumi
Roma ndiyo kitovu muhimu wa sekta ya viwanda na sekta ya huduma ya Italia. Utalii ni pia muhimu sana kiuchumi, kutokana na 26,100,000 watalii wanaoutembelea kwa mwaka: 6.5% za Jumla ya Pato la Taifa zinapatikana ndani ya Roma ambazo ni kushinda miji yote mingine ya Italia.
Roma ina makao makuu ya F.A.O. (Food and Agriculture Organisation - Shirika la Chakula na Kilimo) ya Umoja wa Mataifa pamoja na ofisi zote za serikali ya Italia.
Wakazi
Roma ilianza kama muungano wa vijiji vidogo vyenye wakazi mamia kadhaa. Katika karne ya kwanza BK ilikuwa tayari na wakazi milioni moja. Tangu kuondoka kwa makao makuu ya Kaisari na kupungua kwa nguvu ya Dola la Roma katika magharibi idadi ya wakazi ilipungua hadi kuwa na takriban 100,000 mnamo mwaka 530 BK. Katika karne zilizofuata Italia pamoja na Ulaya iliona vita na mashambulio ya makabila ya washenzi. Mnamo mwaka 1000 BK Roma ilikuwa mji mdogo wa wakazi 20,000 pekee walioishi ndani ya maghofu ya mji mkubwa wa kale. Tangu kuimarika kwa utawala wa mapapa mji ulianza kukua tena mnamo mwaka 1900 Roma ikawa na wakazi 400,000. Katika karne ya 20 BK mji ulipanuka sana hadi kufika idadi ya wakazi wa zamani hata kuipita. Asilimia 7.4 ni wageni.
Orodha inayofuata inaonyesha makadirio hadi 1858, baadaye ni namba za sensa.
|
|
Viungo vya nje
- (Kiingereza) Rome (WikiTravel)
- Info-Roma - Info-Rome ni tovuti kuhusu mambo ya kitalii katika mji wa Roma, hasa matukio ya aina mbalimbali, hoteli, maonyesho, nyumba za kumbukumbu na vyakula.
- (Kiingereza) some quick facts about Rome
- (Kiingereza) Satellite image of Rome at NASA's Earth Observatory
- Rome Travel Guide Guide about Rome with touristic informations
- Rome map 360° IPIX PANORAMA
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Roma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |