[go: up one dir, main page]

Vita ya Japani na Urusi ya 1905

Vita kati ya Japani na Urusi ya 1905 ilipiganiwa katika Asia ya Mashariki. Japani ilishinda na Urusi ilishindwa. Ilikuwa mara ya kwanza ya kwamba taifa la Asia lilishinda nchi ya "watu weupe" wa Ulaya tangu zama za kati.

Picha za Vita kati ya Japani na Urusi
Juu: Manowari; Picha kwa mwendo wa saa: Wanajeshi Wajapani, Wanafarasi Wajapani, Manowari 2 za Urusi, Wanajeshi Warusi wakitazama maiti za Wajapani mbele ya Port Arthur
Eneo la vita: Nyekundu ni Manchuria; rasi ya Liaodong inaitwa "Daijan" (katikati ya ramani katika Manchuria kusini upande wa bahari)

Tokeo muhimu ya vita lilikuwa mapinduzi ya Urusi ya 1905 na kupanuka kwa utawala wa Japani katika Korea na China.

Sababu za vita

hariri

Sababu kuu ya vita ilikuwa mashindano ya nchi zote mbili juu ya athira na kipaumbele katika Korea na Manchuria.

Tangu mwisho wa karne ya 19 Japani ilijaribu kupanusha athira yake katika Asia ya Mashariki. Baada ya vita ya kwanza kati ya Japani na China mwaka 1894 jeshi la Japani liliteka rasi ya Liaodong na bandari ya Port Arthur lakini ililazimishwa kuondoka tena baada ya matishio kutoka mataifa ya Ulaya.

Urusi ilitafuta bandari mpya kwa jeshi la maji. Bandari ya pekee kwa manowari kubwa upande wa Pasifiki ilikuwa Vladivostok lakini mji huu ulikuwa kaskazini mno na wakati wa majira ya baridi bahari iliganda kuwa barafu ikazuia mwendo wa meli. Hivyo Warusi walitafuta bandari upande wa kusini pasipo na matatizo ya barafu. Walipatana na China juu ya mkataba wa kukodi rasi ya Liaodong pamoja na bandari ya Port Arthur iliyopo kwenye pwani la Bahari ya China upande wa magharibi wa Korea.

Hatua hii ilikasrisha Japani. Zaidi ya hapo Warusi walianza kuingia katika Korea kwa makampuni ya kibiashara wakakataa kukubali kipaumbele cha Japani katika rasi ya Korea.

Mwisho wa 1903 serikali ya Japani iliamua kuwashambulia Warusi.

Wanamaji wa Japani walishambulia manowari ya Urusi kwenye bandari ya Port Arthur katika usiku wa tar. 8/9 Februari 1904 na wakafaulu kuzamisha manowari kadhaa na kubomoa nyingine.

Wajapani walishinda pia mapigano kwenye nchi kavu hasa mapigano ya Mukden.

1905 Warusi walituma kundi la manowari kutoka Bahari Baltiki kwenda Asia ya Mashariki. Kwenye mapigano ya Tsushima likashindwa kabisa na wanamaji wa Japani.

Amani na baadaye

hariri

Urusi ilipaswa kutafuta amani. Kwa msaada wa Marekani nchi zote mbili zilipatana kumaliza vita. Urusi ilipaswa kujiondoa katika Manchuria na Korea na kukubali maeneo haya mawili kuwa chini ya athira ya Japani.

Japani iliendelea kutwaa na kutawala Korea kama koloni kuanzia 1910.

Katika Urusi habari za kushindwa zilisababisha ghasia ya wananchi na mapinduzi ya 1905.

Viungo vya nje

hariri
WikiMedia Commons 
WikiMedia Commons


  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vita ya Japani na Urusi ya 1905 kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.