Michezo
Michezo ni amali au mazoezi ya kimwili ambayo mara nyingi yana ushindani ndani yake. Yanatendeka kufuatana na kawaida na taratibu maalumu zilizokubaliwa kati ya wachezaji au katika jamii.
Michezo ni ya aina nyingi ikiwemo michezo ya juu angani, majini, kwenye nchi kavu na pia kwenye barafu. Watu hushiriki kwenye michezo kushindania zawadi, kama aina ya mazoezi au kujiburudisha tu.
- Kuna michezo ambayo huhusisha mwili kama vile mbio ambazo huwa na vitengo tofautitofauti, miereka, dodi, kareti, judo, taekwondo, kuruka juu, kuruka urefu, kuogelea n.k.
- Kuna michezo inayohusisha akili kama vile chesi, sarantanji, bao n.k.
- Kuna michezo inayohusisha wanyama kama vile msabaka na mpira wa polo.
- Kuna michezo inayohusisha mashine kama vile mbio za magari, pikipiki, baiskeli, boti na kadhalika.
- Kuna pia michezo inayotumia vifaa kama vile mipira, silaha, viatu na mbao telezi (zijuilikanazo kwa Kiingereza kama skating shoes/roller skates and skating boards) n.k.
Mifano maarufu ya michezo ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa mikono, mpira wa magongo, aina za mbio, mashindano ya kuogelea na kadhalika.
Watu wengi hupenda kutazama mashindano ya michezo. Tabia hii imekuwa msingi kwa wachezaji wanaotekeleza michezo yao si kwa kujiburudisha, bali kikazi na kwa malipo, pengine makubwa ajabu.
Tangu kale watu wamekutana kwa mashindano makubwa ya michezo kati ya jamii, makabila au mataifa. Kati ya mashindano mashuhuri hasa ni Michezo ya Olimpiki iliyofanyika awali Ugiriki wa Kale na sasa inafanyika kwa ushiriki wa mataifa yote duniani kila baada ya miaka minne.
Kwa nchi ya Tanzania michezo inayopendwa sana ni: mpira wa miguu, riadha, mpira wa pete, mpira wa wavu; pia kuna hamasa kubwa kwa watu kusoma magazeti kuhusu michezo ili kupata dondoo na habari muhimu kuhusu michezo mbalimbali inayoendelea huko viwanjani.
Tanbihi
haririTazama pia
haririKwa Kiswahili
haririKwa Kiingereza
haririViungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Michezo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |