[go: up one dir, main page]

Mkoa wa Dar es Salaam

Mkoa wa Dar es Salaam ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana na Mkoa wa Pwani pande zote barani na Bahari ya Hindi upande wa mashariki.

Mahali pa Mkoa wa Dar es Salaam katika Tanzania.
Dar es Salaam miaka ya 1930.
Uwanja wa Taifa
Machweo jijini
Ghorofa ndefu kuliko zote za Afrika Mashariki.
Makao makuu ya Benki kuu ya Tanzania.
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Shamba la Mungu.

Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani.

Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivyo. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393.

Kuna wilaya tano: City (wakazi 1,649,912), Kinondoni (wakazi 982,328), Temeke (wakazi 1,346,674), Kigamboni (wakazi 317,902) na Ubungo (wakazi 1,086,912). Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizo ni za sensa ya mwaka 2022, ambapo kwa jumla idadi ya wakazi ilikuwa 5,383,728 [1].

Wakazi asili wa eneo la mkoa ni Wazaramo ingawa kwa sasa kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji, kuna makabila yote ya Tanzania, mbali ya wageni wengi kutoka nchi mbalimbali.

Majimbo ya bunge

hariri

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri