Mlango wa La Pérouse
(Elekezwa kutoka La Pérouse)
Mlango wa La Pérouse (Kijapani: Mlango wa Soya) ni jina la mlangobahari unaotenganisha visiwa vya Japani na Urusi. Upande wa kusini kipo kisiwa cha Hokkaido (Japani) na upande wa kaskazini kisiwa cha Sakhalin (Urusi).
Unaunganisha bahari ya Japani na bahari ya Okhotsk. Sehemu nyembamba ya mlangobahari ina upana wa kilomita 43. Kina cha maji hakizidi mita 40.
Jina la mlangobahari limetokana na mpelelezi Mfaransa Jean-François de La Pérouse, aliyepita hapa mwaka 1787 akachora ramani ya kwanza ya sehemu hii na kuandika habari zake.