[go: up one dir, main page]

Orodha ya kimataifa ya magonjwa na matatizo ya afya

(Elekezwa kutoka ICD)

Orodha ya kimataifa ya magonjwa na matatizo ya afya (Kiing. International Classification of Diseases and Related Health Problems au Uainishaji wa Kimataifa wa Magonjwa Yanayohusiana na Matatizo ya Afya, kifupi ICD) ni orodha ya magonjwa yaliyopangwa katika utaratibu kufuatana namba zao.

Ni utaratibu unaokubaliwa kote duniani kwa kutaja na kurekodi magonjwa. Orodha hii inatolewa na Shirika la Afya Duniani. Kulikuwa na matoleo mbalimbali na toleo la kisasa ni ICD-10, toleo la 2006. Toleo jipya la ICD-11 inepangwa kwa mwaka 2015.[1], ambayo itakuwa inapitiwa kwa kutumia Web 2.0.[2]

Hii orodha inatumiwa na madaktari, serikali na makampuni ya bima kutaja magonjwa, kukusanya takwimu za sababu za vifo na kupanga shughuli za tiba.

Asili ya orodha hii ni kazi ya daktari Mfaransa Jacques Bertillon aliyetoa mpangilio wa sababu za vifo mwaka 1893 ambako aliorodhesha magonjwa yanasoababsha vifo. Mpangilio wa Bertillon ulisambaa katika nchi malimbali. Baada ya miaka kadhaa ilionekana ya kwamba sayansi ya tiba iliendelea tayari ikaona magonjwa mbalimbali kwa namna tofauti kwa sababu maelezo mapya yalipatikana. Kwa hiyo mikutano ya kimataifa ilitiishwa tangu mwaka 1900 kuagalia upya mpangilio huu.


Marejeo

hariri
  1. WHO ICD-11 Revision information
  2. "WHO adopts Wikipedia approach for key update". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-05. Iliwekwa mnamo 2007-05-05.

Viungo vya Nje

hariri