Historia Kuu ya Afrika
Historia Kuu ya Afrika (kwa Kiingereza w: General History of Africa (GHA)) ni mradi wa UNESCO ulioanzishwa tangu mwaka 1964.
Shabaha ya mradi ni kusahihisha “maelezo mapotovu yaliyokuwa yakieleza umaskini na ushenzi katika bara hili” kwa “kufanya uchunguzi mwafaka wa habari usiokuwa na upendeleo” . Uliona Historia ya Afrika “imeharibiwa mno kutokana na kutokujua na ubinafsi wa watu walioiandika” [1] .
Awamu ya kwanza hadi mwaka 1999 ilikuwa kuandika na kutoa vitabu 8 kuhusu Historia Kuu ya Afrika.
Awamu ya pili tangu mwaka 2009 inalenga kuandaa muhtasari wa historia na vitabu pamoja na misaada kwa walimu wa shule.
Vitabu vya Historia Kuu ya Afrika
haririVitabu vinane vilivyotolewa vimeandikwa na wataalamu mbalimbali kutoka Afrika na nje yake na kutolewa kwa lugha mbalimbali, zikiwa pamoja na Kiswahili[2]. Vimetolewa mara mbili kama juzuu kamili na juzuu lililofupishwa.
Vyote vinane vya juzuu lililofupishwa vinapatikana kwa njia ya intaneti kwenye tovuti ya UNESCO. Hapa tunonyesha nakala za Kiswahili; viungo kwa nakala za Kiingereza zinapatikana kwenye makala pacha ya Kiingereza.
- Kitabu cha kwanza: Mbinu na Historia ya awali
Mhariri mkuu Joseph Ki-Zerbo, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, Kihausa, Kiswahili na Kifulfulde
- Kitabu cha Pili: Staarabu za Kale za Afrika
Mhariri mkuu G. Mokhtar, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, Kihausa, Kiswahili na Kifulfulde
- Kitabu cha Tatu: Afrika kutoka Karne ya Saba hadi Kumi na Moja
Wahariri wakuu M.M. El Fasi na I. Hrbek, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, na Kiswahili
- Kitabu cha Nne: Afrika kutoka Karne ya Kumi na Mbili hadi Kumi na Sita
Mhariri mkuu D.T. Niane, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, na Kiswahili
- Kitabu cha Tano: Afrika kuanzia Karne ya Kumi na Sita hadi Kumi na Nane
Mhariri mkuu B.A. Ogot, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, na Kiswahili
- Kitabu cha Sita: Afrika kwenye Karne ya Kumi na Tisa hadi miaka ya 1880
Mhariri mkuu J.F.A. Ajayi online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, na Kiswahili
- Kitabu cha Saba: Afrika chini ya Utawala wa Wakoloni 1880-1935
Mhariri mkuu A.A. Boahen, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, na Kiswahili
- Kitabu cha Nane: Afrika tangu 1935
Wahariri wakuu A.A. Mazrui and C. Wondji, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, na Kiswahili
Tanbihi
hariri- ↑ Utangulizi wa jumla, uk 1 HKA Kitabu cha Kwanza
- ↑ TUKI-UNESCO, Historia Kuu ya Afrika, I-VIII, Dar es Salaam, 1999, ISBN 9976 911 40 8
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia Kuu ya Afrika kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |