Amoni Abati
Amoni Abati (pia: Amoni Mkuu, Amun, Ammonas au Ammonius Mkaapweke; Mariotis, 295 - Scetes, 357) alikuwa mmonaki wa karne ya 4 aliyeanzisha Kellia, moja kati ya monasteri maarufu zaidi za Misri na labda ya kwanza kabisa.[1]
Alikuwa kati ya mababu wa jangwani walioheshimika zaidi na alitajwa na Atanasi katika kitabu chake juu ya maisha ya Antoni
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Maisha
haririKisha kusukumwa na familia yake aoe akiwa na umri wa miaka 20, alifaulu kumfanya mke wake akubali waweke nadhiri ya usafi kamili kufuatana na maneno ya Mtume Paulo katika 1Kor 7.[3][4]
Waliishi hivyo bila tendo la ndoa miaka 18, halafu wakatengana kwa ombi la mke wake, naye alikwenda huko Scetis na kwenye Mlima Nitria, kusini kwa Ziwa Mareotis, alipoishi miaka 22, akimtembelea mara mbili kwa mwaka[4][5][6] katika monasteri aliyoianzisha mwenyewe nyumbani mwake.
Alishirikiana na Antoni Mkuu na kukusanya wafuasi wake chini ya usimamizi wake. Alifariki kabla ya mtakatifu huyo aliyemuandikia barua[7],yaani kabla ya mwaka 365, kwa sababu humo alisema kuwa "aliona roho ya Amoni ikichukuliwa na malaika hadi mbinguni"[8].
Maandishi
haririKuna Kanuni za Juhudi (κεφάλαια) 17 au 19 zinazosemekana kuwa za kwake[9][10]
Pia kuna Miundo 22 ya Juhudi iliyoandikwa na Amoni huyo au mwingine.[9]
Hatimaye kuna mkusanyo wa barua zake katika Patrologia Orientalis, volume 10/6.[11]
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Christie, Albany James (1867). "Ammonas". In William Smith. Dictionary of Greek and Roman Biography and Mythology. 1. Boston: Little, Brown and Company. pp. 145. http://www.ancientlibrary.com/smith-bio/0154.html.
- ↑ https://catholicsaints.info/saint-ammon-the-great/
- ↑ Sozom. Hist. Eccl. i. 14
- ↑ 4.0 4.1 Socr. Hist. Eccl. iv. 23
- ↑ Pallad. Hist. Laus. c. 7
- ↑ Ruffin. Vit. Patr. c. 29
- ↑ S. Athan. Opp. vol. i. pt. 2, p. 959, ed. Bened.
- ↑ Vit. S. Antonii a S. Athanas. § 60
- ↑ 9.0 9.1 Lambecius, Commentariorum de augustissima bibliotheca Caesarea Vindobonensi lib. iv. cod. 156, No. 6
- ↑ Gerardus Vossius, Biblioth. PP. Ascetica vol. ii. p. 484, Paris 1661
- ↑ St. Amoun's Letters translated to Arabic
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |