[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Goregore

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Phoeniculus)
Goregore
Goregore kijani
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Bucerotiformes (Ndege kama hondohondo)
Familia: Phoeniculidae (Ndege walio na mnasaba na goregore)
Jenasi: Phoeniculus
Jarocki, 1821
Ngazi za chini

Spishi 6:

Goregore (pia golegole), gegemela au vinuka ni ndege wa jenasi Phoeniculus katika familia Phoeniculidae. Hawa ni ndege weusi wenye mkia mrefu na domo refu jekundu au jeusi lililopindika. Mwangani kwa jua manyoya yao yana mng'ao kijani au zambarau wa metali. Kuna mabaka meupe kwa mabawa na mkia. Hupenda kuwa kwa makundi na hupiga kelele pamoja mara kwa mara wakitetea. Inaelekea kama sauti yao ni asili ya jina “gegemela”. Hula wadudu ambao wanawatafuta katika nyufa za miti kama vigong'ota. Jike huyataga mayai 2-4 ndani ya tundu la kiasilia la mti au tundu la zuwakulu au kigong'ota. Baina ya kundi la kama ndege kumi ipo jozi moja tu inayozaa. Ndege wengine wasaidia hawa wawili kutunza makinda.