[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Peter Grain

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Peter Grain, Jaji Mkuu wa Mahakama kuu ya Uingereza nchini China.

Sir Peter Grain (1864 - 1947) alikuwa jaji wa Uingereza ambaye alifanya kazi kule Zanzibar, Misri, Konstantinopoli na China. Alikuwa Jaji Mkuu wa mahakama kuu ya Uingereza nchini China kuanzia 1927 hadi 1933 na pia jaji wa Mahakama kuu ya Weihaiwei kwanzia 1926 hadi 1930.

Grain alizaliwa mnamo 25 Septemba, 1864. Alikuwa mtoto wa John Peter Grain, mfanyabiashara maarufu wa jinai huko London. Aliitwa kwenye hekalu la Middle Temple mnamo Januari 1897.

Grain alifanya kazi yake katika mahakama za uhalifu za jijini London, kama baba yake huko Uingereza miaka 10 iliyopita. Alikuwa mwanachama wa Baraza la Bar kuanzia 1902 hadi 1906. Mnamo 1906 akiwa na umri wa miaka 42, Grain alianza kazi katika Wizara ya Huduma za Mahakama ya Ofisi ya Mambo ya nje Zanzibar.

Mnamo 1921, Grain aliteuliwa kuwa Jaji msaidizi wa Mahakama Kuu ya Uingereza ya China huko Shanghai. Mnamo 1926 aliteuliwa kuwa jaji wa Mahakama Kuu ya Weihaiwei.

Mnamo 1927, alipandishwa kuwa Jaji mkuu baada ya kustaafu kwa Sir Skinner Turner na kupigwa risasi mnamo Februari 1928, Gilbert Walter King akawa msaidizi wake.

Kustaafu na kifo

[hariri | hariri chanzo]

Grain alistaafu kazi yake mnamo 1933 na nafasi yake ilichukuliwa na Allan Mossop. Alirudi Uingereza na akafariki mnamo 6 Mei 1947, huko Farnham akiwa na umri wa miaka 82.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Peter Grain kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.