[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Pankrasi wa Roma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Pankrasi.

Pankrasi wa Roma (kwa Kigiriki: Παγκράτιος, Pankratios, yaani "Anayeshika vyote"; kwa Kilatini: Pancratius; Synnada, Frigia, leo nchini Uturuki, 289 hivi - Roma, Italia, 12 Mei 303-304) alikuwa mvulana wa Dola la Roma ambaye aliongokea Ukristo akakatwa kichwa kwa sababu ya imani yake mpya[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini. Kwenye kaburi lake Papa Simako alijenga basilika maarufu ambapo Papa Gregori I alikusanya mara nyingi waumini ili wajifunze upendo wa kweli[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Mei[3], siku ya mazishi yake.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. San Pancrazio Martire
  2. Martyrologium Romanum
  3. Calendarium Romanum (Libreria Editrice Vaticana), p. 123

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.