[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Mwenye heri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mwenyeheri)
"Utukufu wa mwenye heri" ulivyochorwa na Sebastiano Ricci miaka 1693-1694 huko Bologna (Italia).

Mwenye heri ni jina la heshima analopewa Mkristo wa Kanisa Katoliki baada ya kufa na ya kufanyiwa kesi makini kuhusu sifa ya utakatifu alilonalo.

Kwa mfiadini inatosha kushuhudia kwa hakika kwamba aliuawa kwa ajili ya imani au adili lingine.

Kwa Wakatoliki wengine unatakiwa ushujaa wa maadili yake yote, hasa yale ya Kimungu na maadili bawaba, sala na unyenyekevu.

Mwaka 2017 Papa Fransisko aliongeza uwezekano wa mtu kutangazwa mwenye heri kutokana na tendo la kishujaa la kuhatarisha uhai wake na kufupisha maisha yake kwa sababu ya upendo.

Njia hizo zote tatu zinatakiwa kuthibitishwa na muujiza mmoja uliofanywa na Mungu kwa maombezi ya mtumishi wake baada ya kifo chake.

Asili ya hatua hiyo ni karne XIV ambapo Papa alianza kukubali marehemu aheshimiwe kwa namna ya pekee mahali fulani au katika shirika fulani kabla kesi ya kumtangaza mtakatifu kwa Kanisa lote haijakamilika.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwenye heri kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.