[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Oka (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Oka)
Oka inapoishia kwenye Volga kwenye mji wa Nizhniy Novgorod
Mwendo wa mto Oka katika beseni ya Volga

Mto Oka ni tawimto wa mto Volga yenye urefu wa kilomita 1,480 katika sehemu ya kiulaya ya Urusi. Ni tawimto mkubwa wa pili ya Volga baada ya mto Kama. Tawimto muhimu zaidi ni mto Moskva.

Mto unaanza katika mkoa wa Oryol Oblast na kuishia katika Volga kwenye mji wa Nizhniy Novgorod.

Oka inapitika kwa meli kwenye urefu wa kilomita 1200. Imeunganishwa kwa njia ya mito mingine na mifereji na Bahari ya Kaspi, Bahari Baltiki, Bahari Nyeusi na Bahari Nyeupe.

Katika historia ilikuwa njia kuu ya usafiri wa mizigo kutoka Moscow (kupitia tawimto wake wa Moskva) hadi kujengwa kwa reli za Urusi.

Wikimedia Commons ina media kuhusu: