[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Macbeth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya tamthilia ya Macbeth.

Macbeth ni tamthilia ya William Shakespeare inayohusu mauaji ya mfalme na athari yake. Ni tamthiliya fupi kabisa ya Shakespeare inayoaminika kuandikwa kati ya miaka 1603 na 1607.

Wahusika

[hariri | hariri chanzo]
  • Duncan - Mfalme wa Scotland
    • Malcom - Mwana wa kwanza wa Duncan
    • Donalbain - Mwana wa mwisho wa Duncan
  • Macbeth - Mkuu wa jeshi la Mfalme Duncan, na baadaye alikuwa Mfalme wa Scotland
    • Lady Macbeth - mke wa Macbeth, na baadaye Malkia wa Scotland
  • Banquo - rafikiye Macbeth na mmoja wa jeshi la Mfalme Duncan
    • Fleance - mwana wa Banquo
  • Macduff - Kiongozi wa jiji la Fife
    • Lady Macduff - mke wa Macduff
    • Mwana wa Macduff
  • Ross, Lennox, Angus, Menteith, Caithness - Viongozi
  • Siward - Kiongozi wa Northumberland, Mkuu wa majeshi ya Kiingereza
    • Young Siward - mtoto wa Siward
  • Seyton - mtumishi wa Macbeth
  • Hecate - Mchawi Mkuu
  • Witches - Wachawi wengine
  • Porter - Askari anayechunga nyumba ya Macbeth
  • Scottish Doctor - daktari wa Lady Macbeth
  • The Gentlewoman - mfanyikazi

Kuhusu tamthilia hii

[hariri | hariri chanzo]
Macbeth pindi anapokumbana na wachawi

Tamthilia hii inaanza pindi wachawi watatu wanapokutana kujadiliana siku ambayo wataonana na Macbeth. Kuna radi na umeme. Baadaye, jeshi la Macbeth limeshinda vita dhidi ya jeshi la Norway. Macbeth, ambaye ni mkuu wa jeshi, anasifiwa kwa kazi yake.

Baadaye, Macbeth na Banquo wanakutana na wachawi watatu wanaomwambia Macbeth kuwa atakuwa kiongozi wa "Glamis" na wa "Cawdor", halafu atakuwa Mfalme. Baada ya muda kidogo tu, Ross, ambaye ni mtumwa wa Mfalme, anakuja kwa Macbeth na kumpa habari kuwa ametuzwa kwa kuwa Kiongozi wa "Cawdor". Maneno waliyosema wachawi yalianza kuwa ya ukweli. Papo hapo, Macbeth anafanya tamaa na kuwa na hamu ya kuwa Mfalme.

Kisha, anamwandikia mkewe barua kumwelezea kuhusu taarifa ya wachawi. Lady Macbeth anatunga njama ya kumuua Mfalme Duncan ili mumewe aupate ufalme. Ingawa Macbeth anaogopa kumuua mfalme, Lady Macbeth anamhimiza kwa kuchokoza ujanadume wake. Macbeth anakubali njama hii.

Usiku wa ziara ya mfalme katika nyumba ya Macbeth, Macbeth unamuua Duncan. Kulingana na mpango wake, anawasingizia watumishi wa Duncan waliolala kwa kuwawekea visu vilivyotapakaa damu.

Mapema asubuhi iliyofuata, Lennox, ambaye ni diwani, na Macduff, ambaye ni kiongozi wa Fife, wanawasili. Askari anawafungulia mlango, kisha Macduff anapatana na maiti ya Duncan huko ndani ya nyumba. Kwa hasira za unafiki, Macbeth anawaua walinzi kabla ya wao kujitetea. Macduff anashuku vitendo vya Macbeth, lakini hasemi kitu. Watoto wa Duncan wanakimbia nje ya nchi kwa hofu ya maisha yao. Macbeth anakuwa Mfalme wa Scotland.

Macbeth anawatuma watu wawili kuwaua Banquo na Fleance. Watu hawa wanamuua Banquo, lakini Fleance alitoroka. Baada ya muda, Macbeth hana raha kwa vitendo alivyovifanya. Macbeth anamshuku Macduff, hivyo basi anamuua mkewe Macduff na watoto wake.

Lady Macbeth anababaishwa na vitendo vya kikatili walivyofanya yeye na mumewe, mpaka akiwa usingizini, akiongea akisema mambo aliyoyafanya ilhali akiwa amelala.

Lady Macbeth akitembea akiwa usingizini.

Macduff anapata habari ya kuwa watu wake wameuawa. Kila mtu sasa anajua kuwa Macbeth ni katili. Malcom anaongoza jeshi la kwenda kupigana na Macbeth. Lady Macbeth anajiua.

Katika vita, jeshi la Macbeth linashindwa. Macbeth anagundua kuwa wachawi wamempotosha. Tamthilia inaisha pindi Macduff anapomkata kichwa Macbeth.