[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Ini Edo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ini Edo

Iniobong Edo Ekim (amezaliwa 23 Aprili 1982) ni mwigizaji wa Nigeria.

Ini Edo alianza kazi yake ya uigizaji filamu mwaka wa 2000, [1] na ameshiriki zaidi ya filamu 100 tangu kuanza kwake. Mnamo 2013, Ini Edo alikuwa jaji wa Miss Black Africa UK Pageant. Mnamo 2014, Miss Ini Edo aliteuliwa na Umoja wa Mataifa kama Mjumbe wa Vijana wa Umoja wa Mataifa wa Habitat .[2]

Maisha ya mapema na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Ini Edo ni mtu wa Ibibio jimbo la Akwa Ibom sehemu ya kusini mwa Nigeria, si mbali na Calabar. Mama yake alikuwa mwalimu, na baba yake mzee wa Kanisa. Ini Edo alilelewa kwa ukali, na ni mtoto wapili kati ya watoto wanne, wasichana watatu, mvulana mmoja. Alisoma Cornelia Connely College huko Uyo.

Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Uyo ambapo alipata Diploma ya Sanaa ya Theatre. Pia alikamilisha programu yake ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Calabar ambako alisoma Kiingereza. [3] Mnamo 2014 alipata udhamini wa kusomea sheria katika Chuo Kikuu Huria cha Kitaifa cha Nigeria .[4]

  1. "T.I.N MAGAZINE: Actress INI EDO Full Biography,Life And News". www.takemetonaija.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-23. Iliwekwa mnamo 21 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. [http://allafrica.com/stories/201104150068.html "Nollywood meet Bollywood As UN-Habitat Appoints Youth Envoys."
  3. "T.I.N MAGAZINE: Actress INI EDO Full Biography,Life And News". www.takemetonaija.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-23. Iliwekwa mnamo 21 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"T.I.N MAGAZINE: Actress INI EDO Full Biography,Life And News" Archived 23 Desemba 2017 at the Wayback Machine.. www.takemetonaija.com
  4. "Ini Edo Gets University Scholarship & Admission To Study Law At NOUN". 
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ini Edo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.