[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kiunzi nje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kiunzi cha nje)
Kichwa cha sisimizi: Chitini

Kiunzi nje ni ganda au ngozi imara inayobeba na kulinda mwili wa mnyama kwa nje, si kwa ndani kama kiunzi cha mifupa.

Wadudu na arthropodi

[hariri | hariri chanzo]

Ni hasa wanyama wa ngeli ya arthropodi kama vile wadudu, buibui na kaa wenye kiunzi nje imara ya chitini.

Tofauti ni matumbawe ambao wanakaa pamoja kwa vikundi vikubwa ilhali kila mmoja anajijengea kihunzi nje kidogo na viunzi hivyo vinabaki baada ya tumbawe kufa lakini wengine hujenga juu ya viunzi vya watangulizi: hivi kujenga mwamba tumbawe ambaye yamekuwa chanzo cha visiwa vingi.

Kwa mnyama mdogo kiunzi hicho bado ni laini lakini kinazidi kuwa kigumu. Baada ya muda kama mnyama anaendelea kukua ganda hili gumu linakuwa dogo. Hapo wanyama wenye kiunzi nje hutupa ganda na kukuza ngozi mpya itakayokuwa gumu tena.

Watu na kiunzi nje

[hariri | hariri chanzo]

Watu walianza kuiga mfumo wa wadudu kwa kujitengenezea aina ya kiunzi nje.

Tangu kale wanajeshi waliwahi kuvaa suti za chuma au bapa mbalimbali za metali zilizokinga kifua, kichwa na tumbo.

Katika tiba kama mguu umevunjika unafunikwa bendeji ya plasta itakayokuwa mgumu; kwa muda ni ganda la nje linalobeba uzito wa mwili badala ya mfupa unaoendelea kupona.

Katika teknolojia ya kisasa wahandisi wanachunguza suti za kuvaa kwa wajeruhiwa au walemavu zitakazowawezesha kutembea tena.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Biolojia

[hariri | hariri chanzo]

Teknolojia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiunzi nje kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.