[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Ferdinando III wa Castilla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro mdogo wa Ferdinando III (karne ya 13)
Mt. Ferdinando.

Ferdinando III (aliyeitwa kwa Kihispania el Santo, yaani "mtakatifu"; 1199/1201[1][2][3]30 Mei 1252) alikuwa mfalme wa Castilla tangu mwaka 1217, wa León tangu mwaka 1230 na wa Galicia tangu mwaka 1231.[4]

Mtoto wa Alfonso IX wa León na wa Berenguela wa Castilla, aliunganisha moja kwa moja falme hizo mbili na kufaulu kuliko wote waliomtangulia katika kurudisha Hispania kusini kwa Wakristo, ikiwemo miji ya Córdoba na Seville.

Pamoja na kufanya bidii kueneza imani, alitawala kwa busara, akistawisha sanaa na sayansi.

Ferdinando III alitangazwa na Papa Klementi X kuwa mtakatifu mwaka 1671.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyoaga dunia[5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. F. Anson (1998) Fernando III: Rey de Castilla y León Madrid. p.39
  2. R.K. Emmerson, editor, (2006), Key Figures in Medieval Europe Routledge. p.215
  3. Jaime Alvar Ezquerra, editor, (2003) Diccionario de Historia de España, Madrid, p.284
  4. Janna Bianchini (2012), The Queen's Hand: Power and Authority in the Reign of Berenguela of Castile, University of Pennsylvania Press, ISBN 9780812206265
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.