[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kamari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Caravaggio, Wachezakarata, mchoro wa mwaka 1594 hivi.

Kamari (kutoka Kiarabu) ni mchezo wa bahati nasibu unaohusisha pesa au kitu kingine chenye thamani kama tuzo kwa mshindi. Tuzo hilo la kubahatisha ndio lengo la mchezo.

Michezo ya kamari imekuwa biashara kubwa kimataifa, ikiwa na bajeti ya dola bilioni 335 mwaka 2009.[1] Umaarufu wa michezo, kama vile soka, na teknolojia mpya vimefanya kamari kuenea duniani kwa kasi kubwa.

Sheria za nchi zinatofautiana kuhusu uhalali wake.[2][3][4]

Hata maadili ya dini yanatofautiana. Kwa mfano dini ya Uislamu inakataza kabisa moja kwa moja uchezaji wa kamari [5][6][7][8][9]

Matokeo hasi

Tatizo mojawapo kubwa ni kwamba wanaoshiriki michezo hiyo wanahitaji au kutamani sana utajiri, hivyo wakishindwa wanaweza kushawishika kucheza tena na tena hadi kufilisika. Baadhi ya wachezaji wa michezo hii hufikia hata kupata matatizo au ugonjwa wa akili. Kuna tiba za aina mbalimbali za kuwasaidia watu wanaoshindwa kuwa na uamuzi wa kuacha michezo hii kutokana na uraibu.

Kamari yenye matatizo ina dalili nyingi. Wachezaji kamari mara nyingi hucheza tena ili kujaribu kushinda pesa ambazo wamepoteza, na wengine hucheza kamari ili kupunguza hisia za kukosa msaada na za wasiwasi.[10]

Nchini Uingereza, Mamlaka ya Viwango vya Matangazo imekemea kampuni kadhaa za kubashiri kwa matangazo yaliyofichwa kama makala za habari zikidai uongo kwamba mtu fulani alikuwa amelipa madeni na gharama za matibabu kwa kucheza kamari mtandaoni. Kampuni hizo zinakabiliwa na faini zinazowezekana.[11]

Utafiti wa mwaka 2020 katika nchi 32 uligundua kwamba, kadri shughuli za kamari zilivyo nyingi katika nchi fulani, ndivyo bei za soko la hisa la nchi hiyo zinavyokuwa tete zaidi.

Tanbihi

  1. "You bet", The Economist, 8 July 2010. 
  2. "Gambling and the Law®".
  3. Humphrey, Chuck. "Gambling Law US". Gambling Law US. Iliwekwa mnamo 2012-09-22.
  4. "UK Gambling Commission". Gamblingcommission.gov.uk. Iliwekwa mnamo 2012-09-22.
  5. Bose, M. L. (1998). Social And Cultural History Of Ancient India (revised & Enlarged Edition). Concept Publishing Company. uk. 179. ISBN 978-81-7022-598-0.
  6. Berel Wein. "Gambling". torah.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-16. Iliwekwa mnamo 20 Julai 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Kucharek, Rev. Cass (1974). To settle your conscience a layman's guide to Catholic moral theology. Our Sunday Visitor. ISBN 0-87973-877-4.
  8. "Blaise Pascal: Mathematician, Physicist and Thinker about God, [[Donald Adamson]] (1995)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-11. Iliwekwa mnamo 2021-12-30.
  9. "International Association of Gaming Regulators: Members". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-11-16. Iliwekwa mnamo 2015-08-20. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  10. "Symptoms and causes". Mayo Clinic.
  11. Betting firms could be fined over ads 'targeting vulnerable people' The Guardian

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kamari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.