Lenzi ya Google hukuwezesha kutafuta unachoona, kufanya mambo haraka zaidi na kuelewa ulimwengu unaokuzingira—kwa kutumia tu kamera yako au picha.
CHANGANUA NA UTAFSIRI MAANDISHI Tafsiri maneno unayoyaona, hifadhi kadi ya biashara kwenye anwani zako, ongeza maelezo ya matukio yaliyo katika bango kwenye kalenda yako na unakili na kubandika misimbo changamano au aya ndefu kwenye simu yako ili uokoe muda.
TAMBUA MIMEA NA WANYAMA Tambua mmea ulio nyumbani kwa rafiki yako au aina ya mbwa uliyemwona katika bustani.
GUNDUA MAENEO YALIYO KARIBU NAWE Tambua na upate maelezo kuhusu maeneo maarufu, mikahawa na maduka. Angalia alama, saa za kazi, taarifa za kihistoria na mengine mengi.
TAFUTA MWONEKANO UNAOUPENDA Je, umeona mavazi yanayokuvutia? Au kiti ambacho kitafaa sana sebuleni mwako? Tafuta mavazi, samani na mapambo ya nyumbani yanayofanana na yale uliyoyaona.
FAHAMU UTAKACHOAGIZA Angalia vyakula maarufu kwenye menyu ya mkahawa kulingana na maoni yaliyotolewa kwenye Ramani za Google.
CHANGANUA MISIMBO Changanua kwa haraka misimbo ya QR na misimbo ya mistari.
*Inapatikana katika baadhi ya lugha na maeneo tu. Kwa maelezo zaidi, tembelea
g.co/help/lens. Baadhi ya vipengele vya Lenzi vinahitaji muunganisho wa intaneti.